Flora amejifungua salama mtoto wa kike siku ya jana saa moja jioni katika hospitali ya Marie stopes na kutimiza ahadi waliyoitoa kwa kumpa mtoto wao jina la Tanzanite.
Anasema ameamua kumuita mtoto wake jina hilo kwa sababu anajivunia nchi yake Tanzania yenye madini Tanzanite yanayopatikana nchini pekee.
Mamu Africa blog ilipomuuliza anajisikiaje kufungua uzazi kwa kupata mtoto wa kwanza mwenye jinsia ya kike akasema "Kwangu ndio nilikuwa naomba nipate mtoto wa kike kwa sababu ya mama yangu mzazi kwani kafurahi kuliko sisi hapa..kwa pamoja tunawashukuru wote waliotuombea mazuri Mungu awabariki"
Mamu Africa blog inawapa hongera H.baba na Flora kwa kumpata Tanzanite na kumtakia afya njema pia.


0 Maoni:
Toa Maoni