Jack amesema mapungufu kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo ya filamu imekuwa kikwazo cha mafanikio kwa baadhi ya wasanii ambao wameishia kujikweza mbele za watu na kufungua Bar za milioni mbili na kujiona ndio wamepata mafanikio makubwa kitu ambacho sio sahihi.
Amesema kutojitambua kwa wasanii ndio chanzo cha utitiri wa filamu zinazotoka kila mwezi ambazo zimekuwa chanzo cha kuwaporomosha wasanii hao wanaoona ufahari,matokeo yake wanaonekana hawana jipya mbele ya jamii kila wanapotoa filamu zao na kuharibu hata soko la filamu,kwakuwa wasanii wote wanaonekana hawana jipya.
"Ninachokiona ni kutojitambua kwa wasanii ndio chanzo cha haya yote ya kuachia movie kila mwezi bila kujua madhara yake,sasa nawashauri wasanii kurudi darasani na kuongeza elimu kwasababu wasanii wengi ni uneducated,hapa inabidi usiangalie u Superstar wako angalia kazi yako zaidi na faida ya kurudi darasani itakayokoa hata soko la hizi filamu zetu"alisema Jack.
Jack ameongeza kuwa hata kuwa na uongozi wa kukuonesha njia na kufuatilia kazi zako nalo ni jambo ambalo wasanii wanatakiwa kulitazama kama kweli wanataka mafanikio na maendeleo ya tasnia ya filamu nchini.
Akizungumzia kwa upande wake,Jack amesema anashukuru muongozo anaoupata kutoka kwa mume wake kipenzi Gadner Dibibi ambaye wamekuwa wanashauriana naye mambo mengi ya maendeleo na amekuwa akimuongoza vizuri katika kazi zake kiasi cha kujiona ni mwenye bahati kumpata mume huyo na hata sasa ameanza kunenepa na kupata afya bora zaidi.
Anasema kwa mwaka kupitia kampuni yake anafanya movie mbili za ukweli zitakazoteka soko la filamu kama ambavyo kwasasa anajiandaa kutoka na bonge moja la movie linaloshirikisha wasanii wa Tanzania,Kenya,Uganda na Rwanda.
Mamuafrica blog inamtakia kila lakheri Jack Pentzel(Kauthar Dibibi) katika safari yake ya mafanikio na kwa kuanza kujitambua.


0 Maoni:
Toa Maoni