May D kama Madee vile..

Mafanikio yanaendelea kuchukua nafasi yake kwa wasanii nchini Nigeria na sasa ni zamu ya Mr. May D ambapo amenunua mjengo wa maana uliomgharimu pesa za ki-Nigeria Naira milion 150.

May D ameshahamia kwenye mjengo wake huo huko Magodo nchini Nigeria wenye vyumba sita na nafasi ya kutosha. Cheki Picha ya nyumba yenyewe.

Hivi karibu msani wa Bongo Madee Seneda alionyesha nyumba yake iliyopo maeneo ya Mbezi ya Kimara kwa mujibu wake ameijenga kwa miaka minne sasa na imemgharimu zaidi ya milioni 125(kama sikosei) na anatarajia kuhamia kwenye birthday yake April 23 mwakani.
Haya ni mafanikio kutokana na muziki,hongera kwa Madee na May D kwa kutumia mafanikio yao vizuri na kwa manufaa.

0 Maoni:

Toa Maoni