Miss Tanzania kuzawadiwa gari ya milioni 15


MSHINDI wa taji la urembo la Miss Tanzania mwaka huu anatarajiwa kuondoka na gari dogo lenye thamani ya Shilingi milioni 15, huku akipewa kitita cha fedha taslimu Shilingi milioni 8.

Mbali na mshindi kutwaa zawadi hizo, mshindi wa pili atapata Shilingi milioni 6.2, mshindi wa tatu shilingi milioni 5,mshindi wa nne Shilingi milioni 3, mshindi wa tano Shilingi milioni 2, mshindi wa sita hadi 15 watapata Shilingi milioni 1.2 kila mmoja na waliobaki watapata Shilingi laki 7 kila mmoja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji amesema mashindano hayo kwasasa yamezidi kukua baada ya kufanyika kazi kubwa kuyafikisha hapo.

Taji la Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred aliyelitwaa taji hilo mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja na kitita cha Shilingi milioni 8.
Nafasi ya pili katika shindano hilo alikuwa Eugene Fabian kutoka Kanda ya Ziwa, Edda Sylvester aliyekuwa Miss Temeke akishika nafasi ya tatu, ya nne ikienda kwa mrembo kutoka Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya tano ikienda kwa Happyness Daniel kutoka Kanda ya Ziwa.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 21, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, na litapambwa na burudani mbalimba za wasanii wa ndani na na mmoja wa wasanii kutoka nje.

0 Maoni:

Toa Maoni