Baba ambaka mwanae hadi kumzalisha imetokea Bagamoyo!

Katika hali isiyo ya kawaida, Mzee mmoja wa makamo Mkoa wa Pwani Wilayani Bagamoyo (Jina Tunalo), amembaka mtoto wake na kumzalisha mtoto huku ndugu, jamaa na marafiki wakiweka vikao na kuyamaliza! MamuAfrica Blog inashuka nayo.

Mzee huyo ambaye katika mahojiano na mwandishi wetu, Edson Mkisi Jr, alikanusha madai hayo, inadaiwa alianza kumfanyia mchezo mchafu mtoto huyu tangu akiwa na miaka nane.
"Mtoto huyo alikuwa akiogopa kusema kutokana na vitusho alivyokuwa anapewa na baba yake na watu walikuja kugundua baada ya kupata ujauzito!," alisema mmoja wa majirani wanaojua tukio hilo.

Aliendelea kusema kuwa habari za mtoto huyo kutembea na baba yake zilikuja kujulikana baada ya kubanwa na mama yake na ndipo aliposema kwamba mimba ile ilikuwa ya baba yake!
"Baada ya hapo baba hakuwa na lakufanya zaidi ya kukiri na kuomba radhi ambapo vikao viliwekwa na kulimaliza hilo tukio," anasema.

Aidha, mama mzazi wa binti huyo alipoongea na mwandishi wetu, alisema tukio hilo ni kweli lilitokea ingawa binti yake huyo kwa sasa ni mke wa mtu na anawatoto wanne.
"Hakuna mtu asiyejua hilo tukio hapa kijijini na huyo mtoto kwa sasa ni mke wa mtu na anawatoto wanne akiwemo huyo ambaye alizaa na baba yake," alisema mama huyo kwa huzuni.

Aliongeza kuwa hata mwanaume ambaye alikwenda kumuoa mtoto huyo walilazimika kumdanganya yule mtoto wa nani ili kuondoa aibu kubwa ambayo kama angeijua huenda uwamuzi wake wa kumuoa mtoto huyo ungemalizia hapo."Tusingeweza kumwambia kama yule mtoto amezaa na baba yake ilibiti tumfiche ili amuoe na hadi leo hajui kama yule mtoto mkewe alizaa na baba yake," alisema.

Balozi wa eneo hilo Bw. Sikujua pia alithibitisha kufahamu kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kwamba mbali na tukio hilo Mzee huyo kwa sasa amekuwa na ugomvi mkubwa na mkewe likihusiana na mzee huyo kugoma kulala chumba kimoja na mkewe.

Kwa tukio kamili,sauti za mashuhuda,baba aliyefanya unyama huu na mama wa mtoto sikiliza kipindi cha Hatua Tatu leo jumatatu na kesho kupitia Times fm 100.5.

0 Maoni:

Toa Maoni