Batuli atangaza yeye ni single lady.....kumbe alishawahi kuolewa!

Msanii wa filamu nchini mtoto mzuri BATULI amefichua siri kuwa aliolewa na umri mdogo wa miaka 16 lakini kwasasa ametangaza kuwa yuko single na milango iko wazi kwa anayetaka kutangaza ndoa.

Batuli ambaye amechanganya asili ya Ethiopia na Tanzania anasema kuwa alilazimika kuolewa katika umri huo na akaitumikia ndoa yake iliyotoa jibu la mtoto mmoja kabla ya baadaye kuongeza mtoto mwingine nje ya ndoa.

Anasema kwasasa yeye ni sigle lady na bado hakuna aliyejitokeza kutangaza ndoa licha ya uzuri alionao ambao anauamini kuwa unaweza kumtetemesha mwanaume na akatangaza kutaka kumuoa.

"Mpaka sasa mimi nipo single kama kuna mwanaume yeyote anayebisha kuwa siko single ajitokeze na aseme kama yeye ndio mpenzi wangu au anamfahamu mpenzi wangu,nakwambia kweli nipo single na ninajijua mimi mzuri kwasababu nazipata sifa za uzuri wangu hata kwa watoto na kila sehemu ninayokwenda,lakini bado hakuna aliyekuja kusema anataka kunioa"alisema Batuli.

Anasema akipata nafasi ya kuolewa atahakikisha haachwi na mume atakayemuoa kwasababu kwasasa anajitambua akiwa na miaka 27 tofauti na wakati anaingia kwenye ndoa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 16,akielezea ni kama aliingia kwenye ndoa akiwa mtoto.

Batuli anasema kutokana na uzuri wake hata kwenye sehemu nyingi amekuwa anakutana na changamoto ya watu kumtaka kimapenzi ikiwemo kwenye tasnia yao filamu anayoitumikia lakini amekuwa na msimamo wake na wanagonga mwamba.

Anasema inawezekana wanaume wanaojitokeza kumtaka wanatofautiana mtazamo kwasababu wao wanatazama leo wakati yeye anatazama kesho katika mahusiano na hayupo tayari tena kuingia kwenye penzi la matamanio au penzi la muda wakati tayari ana watoto wawili ambao wanamtazama yeye.

Anasisitiza yeye ni single lady lakini akaacha milango wazi na ruksa kwa mtu yeyote kugonga hodi naye atamkaribisha kama atafikia vigezo vyake.

0 Maoni:

Toa Maoni