Kriss Jenner (Mama Kim K) na mumewe ndoa imekuwa ndoano!

Baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 22 Kriss Jenner ambaye ni mama wa Kim Kardashian na mumewe Bruce Jenner wametangaza kutengana rasmi kwa mujibu wa mtandao wa Eonline.com.

''Tunaishi tofauti yaani tumetengana na tuna furaha kuwa hivi..'' wameiambia E News.. ''Lakini tutaendelea kupenda na kuheshimiana milele japo tumetengana,tutaendelea kuwa marafiki wa karibu na kama ilivyo kawaida familia yetu itaendelea kupata kipaumbele namba moja.''

Kris na Bruce wamefanikiwa kupata watoto wawili warembo katika miaka hiyo 22 ya uhusiano wao ambao ni Kyle na Kendall na wote wana watoto wanne wanne katika ndoa zao zilizopita.


Pia inasemekana wameishi tofauti kwa muda sasa mpaka walipoamua kuweka mambo hadharani hivi sasa.

0 Maoni:

Toa Maoni