Kumbe Kim K kujitundika na bikini mtandaoni ni mpango!

Imefahamika picha alizopiga mwadada mwenye mvuto Kim K akiwa na vazi la kuogelea tu na kisha kuzitundika katika mtandao ni mpango uliopangwa kati yake na baba watoto wake Kanye West!



 

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichozungumza na Life & Style magazine,Kim K amekuwa akifanya mazoezi ya nguvu kurudisha figure yake na baada ya mambo kukaa vizuri alipiga picha nyingi na kusubiria muda muafaka wa kuzirusha kwenye mtandao baadae kwa pamoja na Kanye waliamua kuchagua moja na ku-share na mashabiki.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamekerwa na kitendo hicho na kumpa makavu bidada huyo kuwa keshakuwa mama hapaswi kupiga picha za aina hiyo na kuzianika kwenye mtandao.

0 Maoni:

Toa Maoni