Mtoto wa mwanamuziki Wahu aponea chupuchupu Wastegate

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Wahu Kagwi 'Wahu' ambae pia ni mke staa wa muziki kutoka Kenya Nameless ame-share story jinsi binti yake wa kwanza alivyonusurika na shambulio la Westgate.

 Kupitia blog yake Wahu amefunguka ilivyokuwa..

Binti yangu alitakiwa kuwepo Westgate kwa ajili ya michezo ya watoto  lakini asubuhi hiyo mama wa rafiki yake akapiga simu na kubadilisha tarehe bila kujua ambacho kingetokea mbele..wakati naangalia TV sikuwa naacha kulia! nililia kwa huruma ya waathirika pia kwa kufikiri huenda na binti yangu angekuwa pale kwenye tukio.. Ameandika Wahu.


Baada ya kuona stori hii ya Wahu nikafikiria mbali sana..Kuna wakati unaweza kuwa  na jambo lako linashindikana kutekelezeka kwa wakati,pengine lilikuwa la haraka kwako au lina umuhimu sana mwisho wa siku tunaishia kulaumu sana bila kujua Mungu kakuepusha na nini mbele yako,kila jambo unalofanya likiwezekana ama kushindikana usiache kumshukuru Mungu maana huwezi kujua kakuepusha na nini. Hapo ki-binadamu unakuta ushajipanga mwenyewe kumpeleka mtoto ku-enjoy safari ilivyoshindikana ukaongea ukalaumuu!

0 Maoni:

Toa Maoni