Wema Sepetu tena..safari hii na mapishi!

Mrembo kiwango Tanzania asiyekaukia katika vichwa vya habari na midomoni kwa watu Wema Sepetu amejitetea anajua sana mapishi baada ya mashabiki kuwa na wasiwasi nae.

Mapema jana Wema alitupia video inayoonyesha anapika wali lakini maoni ya wananchi yalimtuhumu kuwa hajui kupika ni muuza sura tu!!
Haya nishapika mboga baada ya kubandika sufuria ya wali tu ona inavyo harlem shake... mmmmmmh (Post hii ndio iliyosababisha mashabiki kumshambulia)
Baada ya kukamilisha mapishi Wema alijibu mapigo kwa kupost picha ya misosi aliyopika na ujumbe chini yake wenye utetezi.
  ''Jamani najua kupika tena saaaaana.... I was raised in a very good family nd my mom katufundisha wote kupika... dont think sijui... I felt so bad nilivyopost dat video kuna watu waka doubt if I can cook... I cook mashallah sijisifii... so yeah... hahahha mpaka nikarudi nyuma kwenye my posts za zamani... sipendagi tu kujifagilia but kupika tu usiniulize..... hihihihi'' Aliandika Wema.

0 Maoni:

Toa Maoni