Wizkid aanikwa baada ya kufichaficha mambo!

Star boy Wizkid msanii anayeiwakilisha Nigeria imebainika kuwa ni baba wa mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka miwili Boluwatife baada ya kipindi cha nyuma kukana tetesi za kumtia mimba denti na kuwa na mtoto.
 Vishukuriwe vyombo vya habari kwa kuibua mambo ambapo mwaka jana mtandao wa NET uliandika habari kuwa Wizkid kamzalisha mwanafunzi na Wizkid akaibuka na kukana tuhuma hizo kwa kuziita ni kichekesho kwa yeye kutuhumiwa kuwa baba!



December 2012 Wizkid alifunguka tena katika Interview kuwa ''Hizo ni tetesi tu na hata kama nina mtoto hicho sio kitu cha aibu badala yake ningeibuka na kusema mimi ni baba,kila mtu anafanya makosa.Sina mtoto popote"

Akizungumza Oluwanishola Ogudugu amesema mwanzo Wizkid alimkataa kabisa na hata alipoibuka kwenye vyombo vya habari na kutoboa siri hiyo hakuna aliyemjali!


Inaonekana sasa Wizkid amekuwa maana kakubali majukumu yake kama baba na hivi karibuni ali-share picha yake na mtoto kuonyesha ajnajivunia kuwa baba!

0 Maoni:

Toa Maoni