Wizkid 'ala za uso' katika tamasha Abuja!

Mmoja kati kizazi kipya cha muziki walioikamata Afrika kwa sasa Wizkid amekula za uso katika Tamasha lililoandaliwa huko Abuja nchini Nigeria baada ya kutumbuiza na viti tu!


Tamasha hilo lililofanyika Internation Conference Centre huko Abuja limezua gumzo na si kutokana na perfomance ya Wizkid bali kutokana na uchache wa wahudhuriaji kitu kilichosababisha viti vingi kubaki vitupu.



Kwa mujibu wa waandaaji,Tamasha hilo lilitakiwa kuanza saa kumi na moja jioni ila mpaka saa tatu usiku asilimia kubwa ya viti vilikuwa vitupu.

Cheki hali halisi ilivyokuwa.


Hata hivyo Wizkid anaonekana kutojali kilichotokea na kupitia account yake ya twitter amefunguka kuwa 'Up! Aint worried aboutt nothing..onthe next to one..owo n wole wa!' maana yake hajali kilichotokea na hiyo "owo n wole wa" inamaanisha "money is coming in' yaani pesa zinaingia!

0 Maoni:

Toa Maoni