B'Hits yajibu madai ya Mabeste kudhalilishwa na kuondoka kwa wasanii.

Siku moja baada ya Mabeste kusikika kupitia chombo kimoja cha habari akidai kudhalilishwa na maelezo yaliyotolewa na C.E.O wa B’Hits Hermy B kuwa msanii huyo amekosa shukrani kwa kuwa alikuwa akisaidiwa na kampuni hiyo kulipia pango la nyumba na mambo mengine kama ndugu.

Uongozi wa B’Hits kupitia COO (Chief Operations Officer) ambaye pia ni mwana sheria Amani Joachim, ameyatolea maelezo ya kina malalamiko hayo kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times fm.

Amani
Lakini pia kiongozi huyo wa B’Hits amefunguka hali halisi ya mambo yalivyo kutokana na jinsi ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini wasanii wanaondolewa B’Hits kunzia wale wa mwanzo hadi hawa walioondolewa hivi karibuni (Vanessa, Mabeste na Gosby).

Haya ni sehemu ya maelezo ya Amani Joachim alipokuwa akifanya mahojiano na Jabir Saleh aka Kuvichaka katika kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times fm.

Je, unalizungumziaje swala la Mabeste kudai kuwa amedhalilishwa na C.E.O wa B'Hits?

Hiyo statement nimeisikia, lakini kiasi fulani inasikitisha. Unajua jinsi alivyoikanusha hiyo statement imetuacha katika eneo la kumfanya C.E.O wetu aonekane kama ni muongo. Ukweli wa mambo ni kwamba vitu vyote vilivyosemwa ni ukweli. Na alivyojaribu yeye kubadilisha hiyo statement kwamba tulete mkataba wa nyumba sijui tulete risiti na nini, ametumia akili ni vizuri.

Kwani we Jabir ni mara ngapi unapoenda kuchukua fedha kwa mtu hiyo risiti ya hicho kitu unachoenda kukinunua inatakiwa iandikwe jina lake ama la kwako wewe japokuwa umechukua fedha kwa mtu?

Vilevile anavyosema kuhusu kodi ya nyumba, kwamba ikiwezekana tuweze kutoa vielelezo kwamba tumelipa kodi ya nyumba kwa sababu sisi ni ofisi. Nashindwa kuelewa kwamba amesahau muda ambao anapiga simu usiku anaomba kuja kukuoa then mnaelewana nyie ki-brother brother. Yaani mpaka sasa hivi sijaelewa kwamba yale mambo tuliyokuwa tunafanya kama mtu na kaka ameshindwa kuyagundua mpaka sasa hivi, sasa hivi anakuja kusema kwamba tuoneshe risiti.

Kama alikua anataka mambo ya kiofisi basi na yeye alitakiwa alete proposal kwamba naomba kitu flani kwa ajili ya kitu flani halafu apangiwe appointment. Halafu bodi ikae isikilize ile request yake, halafu ikishapitishwa ndio na yeye aitwe asign cheque.

Kwa hiyo kama alikuwa anadhani sisi tuna makosa ya kuchukulia vitu vya namna hiyo kwamba ni kishikaji tu huyu ni mdogo wetu, leo hii unakuja kuomba risiti! That’s very weird men, that’s very unusual and it’s a very big surprise.

Ushauri wangu ningependa kumuomba kwamba akae kiukweli kabisa, afunge macho for once na afikirie na akumbuke kila kitu cha huko nyuma kabla hajafungua mdomo wake na kuendelea kusema maneno mabaya against the C.E.O, personally mimi kama Amani.

Kuhusu watu kujiuliza kwa nini wasanii wengine pia waliondolewa hapo awali, na sasa wanatoka wengine na kuonekana kama B’Hits ina matatizo:

Hilo ni swala kubwa ambalo limechafua taswira ya kampuni, na inaonekana kama kwa namna moja ama nyingine kwamba sisi ni wakorofi. Na kwa ufupi ni kwamba inaonekana kama kuna siri labda nyumba ambayo..either tunagombania fedha ama vitu vya namna hiyo ndio maana labda wasanii wamekuwa sio wanaondoka tumekuwa tukiwaondoa, kwa sababu sio kwamba watu wanaondoka, tumekuwa tukiwaondoa.

Lakini kitu ambacho watu hawakijui, nyuma ya hizi cheni nyingi, kofia na nguo nzuri hakuna hata shilingi kumi, hakuna fedha. Kama watu walikuwa wanajua kuwa B’Hits ilikuwa inagombana na wasanii wake kwa sababu ya fedha iliyowahi kuingia wafahamu kwamba hakuna fedha kwa sababu hawajawahi kuleta fedha.

Mpaka sasa hivi tulikuwa tunaangalia future ya fedha huko mbele, lakini hakuna msanii ambaye unaweza kusema ameleta fedha na watu wamekosana kwa sababu ya hiyo fedha. Kwa kweli ni kitu kibaya ambacho naweza kusema kwamba ni ideology ambayo imejengeka kwa watu kwamba watu wamepiga manyimbo mengi na kwenye show watu wanaonekana wamepiga cheni kubwa na nini kwa hiyo unadhani labda pale watu wanapewa big money, ndio maana ikifika huku nyuma labda ndio maana B’Hits imekaa inagombania hela ya show ndio maana watu wameamua kuondoka, kwa kweli tatizo letu na hao wasanii ni kutokuwepo kwa hiyo fedha.

Lakini B’Hits sio mtu alikuwa hafahamu kuwa biashara ya muziki ni ngumu na mara nyingi, na labda muda wote haina fedha, japokuwa kwa watu wengi ambao wamepigana kweli kweli labda miaka kumi labda ndio fedha imeanza kumwagika vya kutosha.

Fedha kwa B’Hits, I can give you..maximum ya ten million. I swear mbele ya Mwenyezi Mungu, ten million kwenye akaunti ya B’Hits ikiingia inaweza ikatumika 3 days kufanyia kazi. Tuna project ambazo zina-cost mpaka dola 1,500 kwa siku tu, we are spending that enough money Jabir na wewe ni moja kati ya watu ambao huwa wanaona hivi vitu hivi unavionekaga. We are spending hadi zaidi ya dola 1,500 kwa project moja. Cha msingi ni kwamba million moja au mbili it’s not a significant amount of money ambayo inaweza kugombanisha watu B’Hits. That’s petty cash and expenditure. Let me tell you that hamna mtu ambae ameshafikia hatua ya kuingiza njuruku ambayo ikafikia hatua ya watu kama sisi kugombana.

So, Sababu inayotufanya watu kama sisi tuweze mwisho wa siku kuwaondoa wasanii, ni kwa sababu…wasanii wengi wanakuwa hawaingizi kipato. Tunakuwa tumekaa pamoja tumepanga plan za aina flani tuweze kuendelea huko mbele. Tukiangalia hela labda ni miaka miwili mitatu, miwili ijayo..mtu ukishakuwa mkubwa si unajua, it’s a future.

Lakini msanii kwa kuwa anajua kwamba hamna significant plan ya kuweza kuingiza hii fedha kwa haraka haraka anavyotaka yeye, anaamua kufanya mambo mengine kinyume na mkataba wenu na mwisho wa siku yanaishia kukuumiza wewe kama label.

Je, kuna usawa wa kufanya biashara kati ya label na wasanii?

What I’m saying is, most of these artists ni wanyonyaji, mtakaa chini mtachekeana mtaproduce wimbo pamoja. Lakini nje ya makubaliano yenu ana makubaliano na watu wengine kama kumi na mbili.

Kwa hiyo anachokitegemea kutoka kwako ni umpatie ule muziki. Ukishampatia ule muziki ana watu wengine kama kumi na mbili ambao wote ametengeneza nao mikataba tofauti tofauti. Na huwezi kutumikia mabwana wawili hata siku moja, labda hao mabwana wakae pamoja wakubaliane. Lakini wewe nimekupa mkataba wako tumekubaliana nahitaji hiki na hiki. Lakini kuna mambo kibao watu wameomba kwa hiyo msanii.

Kwa hiyo hapo kuna kuwa na conflict of interest, na tunapofika kwenye conflict of interest ya wale mabwana ambao tunamsave yule msanii, unakuta hapo ndio mambo yanapoanza kuharibika.

Mimi kama mimi siwezi kukubali hata siku moja kwamba naendelea kukupa tracks na tumekubaliana kwamba fedha itatokea baada ya miaka mitano.

Lakini kwa muda huu I’m gaining something, You look good umevaa cheni nini na una fans wako..I want that fan base iwe ya kwangu and I want my fan base pia iwe ya kwako. Lakini leo hii unachukua track unaenda kutengeneza fan base and you keep it to yourself, ya kwako wewe pamoja na vitu vyako vingine vingine halafu unaniwekea ukuta mimi ambaye nimekupa track. Mimi siko tayari.

Ni ipi picha halisi ya biashara ya Production hapa Tanzania kwa uzoefu wenu katika soko hili kama B’Hits?

Hapa sasa ntakupa siri nyingine kwa nini B’Hits imekuwa ikiwafukuza watu. Katika production hapa Tanzania kumekuwa kuna unafiki especially wa maproducer, kwa kweli mtu anaeumia katika mlengo wote wa usambazi wa muziki…kila mtu anafaidika katika mpango wake, lakini anaeumia ni producer. Producers mara nyingi wamekuwa hawalipwi.

Halafu kuna kitu kinaitwa proceeds, baada ya biashara. Kwamba ule wimbo unapotoka yale mafanikio yanayotokea hapo, producer hapati kitu.

Tofauti ya B’Hits ni kwamba ni watu waelewa, ni watu ambao wameenda shule na wanajua kikomo cha vitu, kuna sehemu inafika tunaweka stop.

Wakati tunaanza production tunaanza kiukweli kitu kinaitwa sifa kilikuwa kitu kizuri sana, kutajwa tajwa kwenye nyimbo ‘Hermy B, Pancho Latinoo’. Lakini imefika sehemu maneno kama Hermy B na Pancho kwenye B’Hits hayakulishi, hayakulipii kodi ya nyumba na hayakuwekei mafuta kwenye gari.

Sasa inafikia hatua mnasema this is enough, you either pay me or hatufanyi kazi, watu wanaokuja wanalipa mambo yanaendelea. Kwa wale mnaowachukua kwenye label ndio mnategemea sasa mnaweka plan za miaka mitatu miaka mitano.

Kwa wao ni muda mrefu sana, lakini kwa sisi kama kampuni, miaka mitano ni michache sana kwa sababu tunajenga kampuni na tunajenga kitu kimoja by the end of the day tunaweza ku-collect kitu kikubwa.

Kwa nini sasa tunawafukuza, ni kwamba mtu anapochukua ile track anaenda kufanyia mambo yake nje ana-gain yeye mwenyewe. Halafu anakuja tena ndani anaanza kukupa kichwa ‘Panchoo, Hermy B wewe ni nooma, Amani unaandika sijawahi kuona mtu anaandika kama hivi’…unajaa kichwa unatengeneza kitu kingine.

Wanachosahau ni kwamba hii kitu tumei-live tokea mwaka 2005,haya maswala ya kuitwaitwa majina, tokea mwaka huo tumekuwa tunaitwa hayo majina.

Lakini ilifika sehemu nimewazoea nikakua, Pancho ameshazoea amekuwa, Hermy ameshazoea amekuwa. Inafikia hatua unajua kushikana mkono na super star haikulipii kodi ya nyumba,haiweki gari yako barabarani. What you need is cash, you need money.

Na hapa nachosisitiza hatugombanii pesa ya show, hapa tunachogombania ni plans zetu za miaka mitano sita mbele, wewe unapoivunja mimi naendelea kuisogeza mbele inakuwa miaka sita miaka saba mbele mimi ntazifikia lini hizo plans? B’Hits sio nyumba ya kawaida ya producer ambaye unaweza kumletea Castle, ukamletea Amarura, au ukamletea Red bull katika studio yake ukategemea atakutengenezea kazi utaondoka. We say No. Hatuangalii sura, hatuangalii talent na hatuangalii umaarufu, we want our plans to work at some points.

Habari kwa hisani ya www.timesfm.co.tz

0 Maoni:

Toa Maoni