Binti ajinyonga baada ya kukatazwa kutumia facebook!

Msichana wa Kihindi mwenye umri wa miaka 17 amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook na kutotumia muda mwingi kwenye simu yake ili aweze kuzingatia zaidi masomo.

Kwa mujibu wa gazeti la Newsweek Pakistan, msichana huyo aliyejulikana kwa jina la Aishwarya Dahiwal anaeishi Parbhani huko India alikutwa amejinyonga chumbani kwake ijumaa ya wiki iliyopita baada ya kugombezwa na wazazi wake siku ya jumatano. 
 
 
Afisa mmoja wa polisi ambae hakutaka jina lake litajwe aliliambia gazeti hilo kuwa polisi walikuta mwili wa msichana huyo ukiwa unaning’inia chumbani kwake, aliacha karatasi yenye maelezo ya chanzo cha yeye kujinyonga kuwa ni kutokana na kugombana na wazazi wake kuhusu Facebook.

“Walimwambia azingatie masomo yake. Baada ya kugombana alijifungia chumbani kwake na baadae akakutwa akiwa amening’inia na karatasi yenye ujumbe ikiwa pembeni yake.”Alieleza Afisa huyo wa polisi.

Baba mzazi wa binti huyo alipoulizwa alisema, “bado hatujaamini, tumepata mshituko mkubwa, tulitaka ajikite zaidi katika masomo, hatukufikiria kuwa angechukua hatua hiyo.”

Bado polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

0 Maoni:

Toa Maoni