Sakata la Dayna na Diamond hapa ndipo lilipofikia..

Maswali mengi bado yako mtaani kuhusu nini kinaendelea kwa upande wa Dayna kuhusu yale malalamiko yake kuwa ‘alipokonywa’ mdundo wa wimbo wake na ukatumika kufanya hit ya ‘My Number One’ ya Diamond Platinumz, ambapo alisema ameipeleka kesi COSOTA, wengi wanauliza ama ni vile alitaka kupata kick na kuipotezea? Ni maswali yaliyoko mtaani. 
 
 
Mwimbaji huyo wa ‘Nivute Kwako’ ameiambia tovuti ya Times fm kile kinachoendelea na kwamba bado swala hilo liko COSOTA na yeye anaendelea kusubiria majibu, lakini anapata mrejesho kidogo kuhusu kile kinachoendelea japokuwa haruhusiwi kuyaongea.

Hata hivyo Dayna ameonesha hali ya kuwa na mashaka kidogo kwa kile kinachoendelea kutokana na mrejesho anaoupata, japokuwa hakuzungumza nini hasa kinampa kigugumizi, lakini sentensi zake zinatoa picha.

“Mambo yetu yamekuwa na process kidogo, japo si kubwa sana, lakini tuombe Mungu..Mungu anaweza akajaalia muda wowote tukafikia muafaka, kwa sababu kwa upande wangu ninachosubiri ni maelezo tu, niitwe labda niambiwe kuna hiki na hiki.” Amesema Dayna.
Habari kwa hisani ya tovuti ya Times fm.

1 comment:

  1. Anatafuta kick mjini. Dayna kwa uanamuziki upi? Amuache Diamond alale. Masikini Dayna mvuto sifuri, kuimba ndio kabisa sasa kaona anyang'ane beat na kipenzi chetu. Kama mziki umekushinda mama kalime. Sio lazima wote tuwe wanamuziki wengine tubaki mashabiki.

    ReplyDelete