Steve Nyerere ajiweka kwenye gari ya milioni 32!

Nyota wa filamu za vichekesho nchini kutoka kiwanda cha filamu Bongo movie Steve "Nyerere"Mengele ameamua kujiweka kwenye gari aina ya Jeep lenye thamani ya shilingi milioni 32.

Nyerere anasema hayo ni moja ya mafanikio ambayo anayapata kupitia filamu yanayomuwezesha kununua gari ya tahamani kama hiyo pamoja na kufanya mambo mengine ya maisha.

Nyota huyo anayejiandaa kuingiza filamu nyingine mpya sokoni anasema gari hiyo ni moja ya mali zake ambazo anamiliki na ambayo ameiweka hadharani.
 
 
 
 
 

0 Maoni:

Toa Maoni