Mrembo Miss Tanzania anusurika kunyongwa kisa dawa za kulevya!

Mrembo aliyewahi kushiriki kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2008 ambaye kwasasa anafanya kazi ya mitindo amenusurika kunyongwa nchini Singapore kwa tuhuma za kuhusika kwenye biashara ya dawa za kulevya.

Mrembo huyo Mariam Bakar aliyevikwa taji la Miss Pwani 2008 baada ya kufanya vizuri kutokea Miss Bagamoyo anadaiwa kuchomewa na marafiki zake wa karibu kuwa anajihusisha na biashara hiyo ya dawa za kulevya,taarifa ambayo pia ilichukua nafasi kwenye vyombo vya habari mbalimbali.

Akisimulia mkasa mzima Mariam anasema baada ya marafiki hao kuona anapata mafanikio wakaamua kumsingizia kesi hiyo ya dawa za kulevya,kesi ambayo ilifika mpaka ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Anasema kwa mujibu wa sheria za Singapore mtu yeyote anayekamatwa na dawa za kulevya adhabu yake ni kunyongwa lakini kwake kwakuwa hakuwa akijihusisha na biashara hiyo akaikwepa adhabu hiyo lakini akakutana na mtihani wa kutakiwa kurudishwa Tanzania na akapewa saa 24 kuondoka katika nchi hiyo.
 
 

Hata hivyo katika hali aliyoiita ni Mungu kusikia maombi yake akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na mbwa wa Polisi alipewa taarifa kuwa yuko huru na anaweza kuchagua nchi anayotaka kwenda.

Mariam anashukuru kwa suala hilo kuisha na sasa anaendelea na maisha yake japokuwa tayari jina lake limechafuka nchini humo na kumchafulia kazi yake ya mitindo ambayo amekuwa anaifanya kwa mafanikio makubwa.
 



0 Maoni:

Toa Maoni