''Kitu kinachofanya tuelewane na kuishi muda mrefu bila matatizo ndani ya ndoa ni mimi kumpa moyo na msukumo wa kuwa anavyotaka kuwa ama kwa lugha rahisi kutimiza ndoto zake na kumpa sapoti kwa asilimia mia moja.
Wanaume wengi wamewafumania wake zao kwa sababu tu ya kuwakataisha tamaa na kutowaruhusu kufanya kile wanachopenda. Huwa Namshauri na kumsukuma mke wangu na watoto kutimiza ndoto zao na kuwa wanavyotaka kuwa.
Kuna wanawake wanapenda kuigiza lakini waume zao hawawaruhusu kwa kuhofia kusalitiwa.Ndoa ni heshima kwa wale wasaliti hata ufanyaje watasaliti tu so kikubwa ni mtu kujitambua''. Alifunguka Captain Mathew.
Ni kweli kama ni mwepesi kutambua mambo utagundua wanaume wengi wamekuwa ni wagumu kuwasapoti wake zao/wapenzi kufanya wanachopenda kwa kuhofia kusalitiwa kitu ambacho naweza kuita ni wivu wa kijinga.Wengi huwakatisha tamaa hata kama mwanamke anaweza atajiona si chochote kitu amabcho ni kibaya sana!
Mpe mkeo uhuru wa kuchagua na kufanya anachopenda kwa sababu kama mnapendana kweli mafanikio yake ni yenu wote so wanaume wa kikwetu mjifunze kutoka na huyu bwana kumbana na kumnyima uhuru mpenzi wako si kumpenda bali nji mambo ya kizamani..kanifurahisha sana bwana Captain lol!


Maneno so luvly jamani maana wengine tunajitayarisha kuomba talaka maana naona maisha hayaendi na yapo nnayoweza kuyafanya tena kihalali but mume hataki bora niwe single parent mie.
ReplyDelete