Wolper hataki maswali ya sababu za kubadili dini!

Mwanadada mrembo kutoka Tanzania anayefanya filamu Jackline Wolper amefungukia sababu zilizomfanya abadili dini na kusema watu waache maswali.

Kupitia mtandao wa Instagram hiki ndicho alichoandika.


'mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote.'

Wolper alibadili dini siku za nyuma kuwa mwislamu na kuitwa Ilham kabla hajaamua kurejea katika dini yake ya zamani yaani ya kikristo.

0 Maoni:

Toa Maoni