Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki Bob Junior au Sharobaro President amesema kuwa hana mpango wa kuoa tena baada ya kuachana na mkewe.
Sharobaro President ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa kutokana na
kusumbuliwa na ndoa yake na kukosa furaha katika maisha ya ndoa, ameamua
kuachana na habari za kuoa na kuishi ki-bachelor kwa kuwa ameona shida
ya ndoa na raha ya kuishi kibachelor.
“I’m single, sitaoa tena…mimi niko single na sitaoa tena. Kwa sababu
nimeona ugumu wa ndoa na wepesi wa kuwa bachelor. Kwa hiyo nimeamua kuwa
bachelor na siwezi kuoa tena, sioi tena jamani I’m single. No more kuoa
Bob Junior” Bob Junior ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Unajua unapokuwa kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend, hamna
ile ‘uko wapi sasa hivi, rudi haraka nyumbani’, umeenda kwenye show
ukirudi mara kanuna.”
Ameeleza kuwa ndoa yake ilikuwa inarudisha nyuma maendeleo ya kazi
yake kwa kuwa katika siku saba za wiki ni siku mbili tu anakuwa na
furaha, na kwa kuwa kazi yake inategemea ubunifu na utulivu asingeweza
kufanya kazi vizuri.
Amesema mkewe alikuwa na wivu na alikuwa akiingilia hadi ukurasa wake wa facebook na kuwatukana watu waliokuwa wanachat nae.
Katika hatua nyingine, Bob Junior ameelezea kuhusu kufuatiliwa mara
kwa mara na baadhi ya magazeti na kumuandika vibaya, ambapo amesema
ukubwa wa jina lake ndio chanzo cha kuandikwa.Amesema amejaribu
kuwakataza lakini anaona wanaendelea.
Kuhusu kuandikwa kuwa ni Freemason katika kipindi cha hivi karibuni, alifunguka:
“Kuna picha ambayo niliweka alama ya Freemason. Kwa hiyo kila
nikijaribu kuwakatalia nashindwa kwa sababu picha inaonesha ushahidi
kwamba mimi niko kwenye hiyo dini, wakati ukweli mimi siko katika dini
hiyo. Kwa hiyo kila siku wanajaribu kutafuta vitu vipya. So nadhani ni
wakati wangu tu ndio maana wanajaribu kuandika hivyo.”
Usikose kusikiliza kipindi cha The Jump Off ya 100.5 Times Fm, na Bongo Dot Home wiki hii kwa undani zaidi wa story hii.
Habari kwa hisani ya tovuti ya Times fm.

0 Maoni:
Toa Maoni