Kama ni mrembo au una shughuli yoyote,Mac saloon wanakuhusu soma hapa!

Kama una Harusi inawezekana ukawa wewe ndio bibi harusi au jamaa yako na unahitaji kupendeza kwa make up za ukweli na original kulingana na ulivyo basi Mac saloon wanakuhusu sana. Si harusi tu kuna Kitchen party,send off au shughuli yoyote unahitaji kurembwa/kupambwa basi usihangaike watembelee hawa wapo Sinza mori karibu kabisa na Meeda.

Mac saloon ndio wamehusika katika kunipamba kwenye harusi yangu,Cheki picha zangu hapo chini na ujionee kazi yao.

Ukitokea Sinza Mori ni baada ya kupita Meeda kidogo,ila ukitokea njia ya Mlimani City unaanza na saloon yao ndio unaelekea Meeda.Pia usiogope kuhusu bei ni nafuu na unaweza kuzimudu pia.


4 comments: