Wagoma mtaa kubadilishwa jina ili kumuenzi Paul Walker!

Kumekuwa na ‘vuta n'kuvute’ kati ya mashabiki wa Paul Walker na wakazi wa eneo ambalo muigizaji huyo wa Fast and Furious alipata ajali na kupoteza maisha akiwa na rafiki yake Roger Rodas, kuhusu kubadili jina la mtaa huo ili kuwaenzi.


 Kundi la fans wa Paul Walker wamepitisha pendekezo hilo na kulipeleka kwenye utawala wa jiji la Santa Clarita huku wakikusanya sahihi zaidi ya laki mbili kwa njia ya mtandao ili kuushawishi uongozi huo kupitisha ombi lao, linalotaka mtaa huo uitwe ‘Walker Rodas Memorial Parkway’.

Hata hivyo wakazi wa eneo hilo wameendelea kupinga ombi hilo wakidai kuwa Paul Walker hakufanya kitu chochote kwa jamii hiyo.

Kiongozi wa halmashauri ya jiji hilo, TimBen Boydston ameiambia TMZ  kuwa mtaa unaweza kubadilishwa jina endapo jamii ya watu wanaishi eneo hilo wataafiki, kwa hiyo inaonekana kama mpango wa kubadili jina mtaa huo ni kama ndoto za mchana.

0 Maoni:

Toa Maoni