Maambukizi ya Saratani inayosababishwa na mapenzi ya mdomo yanadaiwa kuongezeka hapa nchini.
Maambukizi hayo yanaonekana kuongezeka kwa kasi kubwa kwa saratani hiyo inayotokana na maambukizi ya kujamiiana kwa njia ya mdomo na kwa njia ya hewa,hiyo inathibitishwa na takwimu ya idadi ya wagonjwa.
Hospitali ya Ocean Road imekuwa ikipokea wagonjwa wapatao 500 mpaka 600 kwa mwaka hali inayoonesha ongezeko la ugonjwa huo kwa njia hiyo ya mdomo tofauti na awali walipokuwa wakipokea wagonjwa 200.
Mkurugenzi wa Idara ya kinga hospitali ya Ocean Road Dk Julius Mwaiselange amesema kasi ya ongezeko la saratani kwa njia ya mdomo imekuwa kubwa tofauti na miaka iliyopita.



0 Maoni:
Toa Maoni