Kofia aliyovaa Pharell Williams kwenye tuzo za Oscar yageuka bonge la dili!

 
Kofia aliyoivaa Pharell Williams kwenye utoaji wa tuzo za Grammy January 26 mwaka huu iliyogeuka kuwa mada kubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari imepata matunda ya promo hiyo isiyo rasmi na imeweza kuwa bidhaa iliyouzwa $44,100 (zaidi ya shilingi Milioni 71 za Tanzania).

Pharrell alitangaza kupitia Twitter Jumapili, March 2 kabla hajaelekea kwenye tuzo za Oscar na kuonesha kuwa kofia hiyo iliuzwa kwenye mnada wa eBay kwa kiasi hicho huku akimshukuru mtu aliyeinunua.
“Asante kwa yeyote aliyenunua kofia yangu ya Grammy kupitia @eBay kwa $44,100. Mchango wako unanufaisha mkono mmoja kwa mwingine.” Kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili, hivyo ndivyo tweet yake ilivyomaanisha.

Lakini haikuchukua muda akajibiwa na Arbys ambaye tangu mwanzo alikuwa ameiona kofia hiyo ikiwa na mfanano wa logo ya biashara yake.  “You are welcome. We’re HAPPY to support a great cause & get our hat back. Good luck at the #Oscars tonight.” Naye akajibu, “What a plesant surprise. Thank you @Arbys, our roast beef is now officially well done.”

Kofia hiyo ambayo iligeuka topic kwenye Grammy, iliweza kufunguliwa hadi akaunti maalum ya Twitter. Lakini Arbys ambaye hivi sasa ni mmiliki halali wa kofia hiyo alitweet akimtania Pharrell kuwa kama vipi awarudishie kofia yao.
“Hey @Pharrell, can we have our hat back?” Aliandika Arbys.


Haikuchukua muda, Pharell akatangaza mnada wa kofia hiyo. Kofia hiyo iliendelea ku-make headline hata katika tuzo za Oscar Jumapili iliyopita baada ya host wa show hiyo Ellen DeGeneres kutumia kofia kama hiyo kukusanyia pesa kwa watu ikiwa ni sehemu ya huduma yake (tip).    

        

0 Maoni:

Toa Maoni