MAAJABU : Mke na mume wapasuliana vitu vya nyumbani mwilini!

Ni kama aina fulani ya uchizi.....Mume na mke huko Mashariki mwa India wameanzisha mchezo wa hatari na kushangaza...Wanakwenda sehemu ya hadhara na kupasuliana vitu mbalimbali vya nyumbani mwilini mwa kila mmoja!

Picha nyingine zinaonesha nazi ikipasuliwa mgongoni mwa mke lakini nyingine zinaonesha nazi hiyo ikipasuliwa sehemu ya tumboni na karibu na shingo.

Bhramaramba Budati anampa nafasi mume wake kupasua nazi na vitu vingine tofauti kwenye mwili wake mbele ya mkusanyiko wa wana kijiji wenzake huko Andhra Pradesh region.

Jionee mchezo huo wa hatari.
 
 
 
 
 
 
 
 
 

0 Maoni:

Toa Maoni