Mapenzi haya dah..Robin Thickle amlilia mke wake hadharani!

 
Mapenzi yanaendelea kumuumiza mwimbaji wa ‘Blurred Lines’, Robin Thicke baada ya kutengana na mkewe Paula Patton.Mwimbaji huyo ameamua kutumia muda wake anaokuwa jukwaani kuelezea hisia zake kwa Paula na kuwaahidi mashabiki kuwa atafanya jitihada zote amrudishe mkewe.
Jumatano ya wiki hii, mwimbaji huyo hakusita kuweka wazi kuwa anampenda kweli Paula baada ya shabiki mmoja aliyehudhuria show yake hiyo kusikika akisema ‘I love Paula’.
Robin aliitumia sauti ya shabiki huyo kusema neno moja tu la moyoni, kuwa anampenda pia, ‘I do too.’

Baadae aliendelea kutoa hotuba fupi ambayo inaendana kabisa na kile anachokifanya yeye kumsifia Paula japo wametengana.
“Usiache kuamini na usiache kupenda, hata kama mmeachana, hakikisha mnatendeana wema. Itendee mema familia yako. Mtunze mama yako, watunze watoto wako na mambo mazuri yatakujia. Endelea kuamini tu kuwa Mungu ni mwema.”

Ni vigumu sana kwa mtu maarufu kama huyo kumlilia mara kwa mara mwanamke aliyemuacha tena mara nyingi anapokuwa jukwaani ama sehemu zenye watu wengi.
February mwishoni, alifika Washington D.C na kuelezea kuwa anahitaji kuwa na Paula tena.
Lakini kabla hajaanza kuimba ‘Lost Without U’ huko Virginia, alielezea jitihada zake za kumrudisha mkewe huku akimsifia kuwa mke mwema.“Kwa wote msiofahamu mimi na mke wangu tumeachana, lakini najaribu kumrudisha msichana wangu. Ni mwanamke mwema.” Alisema Robin Thicke.

Hata hivyo, chanzo kimoja kiliiambia TMZ kuwa Paula hashitushwi na vilio vya Robin jukwaani, bali anafanya uchunguzi wake mwenyewe kujua ni jinsi gani Robin yuko Royal kwake, na kwamba anatumia zaidi camera za Paparazzi kujua anazunguka na nani na anafanya nini kwa sasa, wakati huo huo anaendelea kufanya mikakati ya kupata talaka yake.

Robin na Paula walikutana wakati Robin ana umri wa miaka 14 tu na wakafunga ndoa mwaka 2005. April, 2010 walibarikiwa mtoto wa kiume anaeitwa Julian Fego.


Ililipotiwa kuwa Robin na Paula walitangaza kutengana baada ya kuonekana picha za Robin Thickle akiwa ‘0-distance’ na msichana mmoja. Lakini pia iliripotiwa kuwa msichana huyo alimkiss Robin na mwisho wakakutana faragha baada ya utoaji wa tuzo za VMAs.

January mwaka huu, FishWrapper iliripoti kuwa mwimbaji huyo alionekana akiwa anacheza vibaya na msichana mmoja huko Paris.
Habari kwa hisani ya website ya Timesfm.co.tz

0 Maoni:

Toa Maoni