Leo MamuAfrica blog inakupa nafasi ya kusoma story ya kusikitisha ya kimapenzi ya Binti mdogo na mrembo Jojo Tsai mwenye umri wa miaka 20 ambaye amejitoa uhai wake baada ya kudai kuwa aliyekuwa mpenzi wake kamdanganya.Inadaiwa kuwa alikuwa akimwambia anataka kumuoa na kupata watoto pamoja kitu kilichofanya Jojo ajenge imani kubwa kwa kijana huyo lakini mambo yakabadilika baada ya kijana huyo wa kichina kudai mama yake hajakubaliana na ndoa hiyo.
Baada ya kuachana, Jojo aliamua kuendelea na maisha yake kwa kuanzia uhusiano na mwanaume mwingine lakini yakashindikana kwani bado alikuwa anampenda sana mpenzi wake aliyepita kwa hiyo kuondoa maumivu akaamua kujiua kwa kuruka kutoka juu ya jengo!
Kabla hajaamua kujiua alipost ujumbe wa kimapenzi kuonyesha jinsi alivyoumizwa moyo na huyo mpenzi wake wa kichina katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha ambazo zinaonyesha akichoma vitu vilivyohusiana na mapenzi yao yaliyopita na baadae akajipiga picha akiwa kakaa juu ya jengo hilo kabla ya kujirusha! Cheki picha chini..
Hakuishia hapo,pia ali-post picha inayomuonyesha mpenzi wake huyo aliomvunja moyo wake..inasikitisha!
Ukurasa wake wa Instagram kwa sasa umejaa balaa kila mtu akiandika jinsi alivyosikitishwa na yaliyotokea huku pia wakimuombea apumzike kwa amani.
Huu ni ujumbe alioucha Jojo kuhusu mpenzi wake huyo:
“Ni siku 12 sasa tangu tuachane.Nimekuwa natoka out,napata chakula na kuangalia movies na wanaume mbalimbali,wengine ni ma-handsome kukuzidi..wengine ni matajiriri kuliko wewe. Nasema haya ili uone ni jinsi gani kuna ugumu kwangu kumpata zaidi yako..moyo wangu hauwezi kumkubaliyoyote! Kila nikitoka nao out najilazimisha kucheka lakini naishia kulia tu..mwisho inabaki siwezi kubadili moyo wangu.
“Maisha yamekuwa mabaya hizi siku.Nataka kusahau yote,kujicontrol nisilie kila usiku lakini imekuwa ngumu kufanya hivyo.Yote haya ni kama ulonevu kwangu..kwa nini umenipa ahadi nyingi? Kwa nini umenidanganya? Sijawahi hata kufanya baya kwako lakini maisha yamekuwa ni kama adhabu kwangu.
Siwezi kusahau haya labda nife. Sikuwahi kufikiri kuwa utanidanganya lakini bado siwezi kuacha kukupenda. Nikifa nitaendelea kukuwinda usiku na mchana..sitawea kutengana na wewe daima.






Da mamu hii strory imeniumiza sana ata mi pia yamenikutana kama haya! Simshangai huyu dada kufanya maamuzi kama haya, R.IP!
ReplyDelete