Bi. Clinton alikuwa akihutubia katika eneo la Mandalay Bay ambapo mwanamke huyo alirusha kiatu ghafla kwa lengo la kumpiga.
Hata hivyo, Clinton alikikwepa kwa ustadi kiatu hicho na kisha kuendelea na maelezo ya utani juu ya tukio hilo.Walinzi walimshika mwanamke huyo na kwenda nae nje na kwa mujibu wa Daily Mail alitupwa selo.
Tukio hilo linafanana na lile la George Bush kurushiwa viatu viwili na mwandishi wa habari alipokuwa akihutubia nchini Iraq mwaka 2008 na alivikwepa viatu vyote viwili.
Habari kwa hisani ya website ya Times fm.

0 Maoni:
Toa Maoni