VIDEO: Mama amshushia kipigo cha mwizi binti yake baada ya kutupia picha facebook!

 
Video inayomuonyesha mama mwenye hasira kutoka Trinidad akimuadhibu kwa kutumia mkanda mtoto wake wa kike mwenye miaka 12 baada ya kutupia picha zisizo na maadili facebook imevuja.

Jumapili iliyopita video hiyo inayomuonyesha Hellen Barlett mama watoto wanne akimcharaza kwa hasira binti yake huyo huku binti  huyo akilia kwa uchungu iliwekwa facebook.


Mama huyo anasema hajutii kumchapa kiasi hicho binti yake na yuko tayari kwenda jela kama itatokea hivyo lakini anataka kuhakikisha binti huyo anaenda katika njia iliyonyooka. Akifunguka zaidi mama huyo anasema tangu baba wa watoto wake alipowatelekeza binti yake amekuwa hashikiki kwa hiyo kama mzazi anahofia kuletewa ujauzito au habari mbaya.

Cheki video hii kisha niambie mtazamo wako kama alichofanya Hellen ndio sahihi na atafanikiwa kulinda maadili ya binti huyo au amechemka na anazidi kumtengenezea usugu binti yake! Ila watoto wa sasa kiboko aisee.. sasa binti wa miaka 12 picha za ajabu facebook na tayari ana ma-boyfriend kwa mujibu wa mama yake!! tutafika kweli?

             

0 Maoni:

Toa Maoni