Khloe apigwa marufuku kutinga na French Montanna kwenye harusi ya 'Kimye'

Familia ya Kardashian kila mara imekuwa inatengeneza vichwa vya habari katika vyombo vya habari na mitandao huko majuu kutokana na vituko na skendo wanazozikwaa kila mara.

Baada ya kuthibitika kuwa sasa Khloe Kardashian anatoka kimapenzi na rapa French Montanna ambaye tayari ana mke, inasemekana kuwa familia yake haijapokea vizuri uhusiano huo yaani dada yake Kim na mama yake hawafurahishwi na hilona kutokana hilo amepigwa mkwara wa kutoenda  rapa huyo kwenye harusi ya dada yake Kim na Kanye West itayofanyika May 24 Ufaransa.


Kwa mujibu ya mtandao wa Rada Online inasemekana Khloe ana mpango wa kuibuka na French Montanna kwenye harusi ya Kim Ufaransa lakini Kim hakubaliani na hilo kwa sababu hampenzi French na anahisi haendani na mdogo wake kwa hiyo hataki kumuona kwenye harusi yake. Pia mama yake Kris Jenner anakubaliana Kim kwa kusema ni mapema sana kwa French kuhudhuria mambo yao kama sherehe za kifamilia.

Khloe anasema uhusiano wake na French sio serious ila tu anataka kujifurahisha na pia kusahau yaliyoyapitia na aliyekuwa mme wake Lamar. Pia anasema itakuwa ngumu kwake kwenda kwenye Harusi ya Kimye peke yake itamrudishia kumbukumbu za ndoa yake na Lamar.

0 Maoni:

Toa Maoni