PICHA: Ronaldo 'auza' utupu wake hadharani!


Mwanasoka mwenye mvuto anayeichezea timu ya Real Madrid ya Nchini Hispania, Cristiano Ronaldo, ametokelezea katika ukurasa wa mbele (front page) kwenye jarida maarufu la Vogue la nchini Hispania akiwa mtupu!

Huku akionekana mwenye mvuto zaidi, Ronaldo, amepozi akiwa kasimama sambamba na mpenzi wake Irina Shayk, ambaye ni mwanamitindo. Mchezaji huyo mwenye kiwango cha juu cha soka ndani ya timu hiyo, ameingia kwenye orodha ya mastaa waliowahi kulipamba jarida hilo katika siku za hivi karibuni.

Jarida hilo maarufu duniani, limekuwa na kawaida ya kuwauzisha 'sura' mastaa mbalimbali huku baadhi ya mastaa hao wakilipwa 'mkwanja' mrefu kutokana na kulipamba jarida hilo maarufu.


0 Maoni:

Toa Maoni