Akizungumza kwa msisitizo na wasanii hao katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, Steve aliwataka wasanii kuweka tofauti zao pembeni na kuuchukuwa msiba huo kama wao kwa lengo la kufanikisha msiba huo.
Akizungumza huku akisikilizwa na wasanii hao, Mwenyekiti huyo alikwenda mbali na kusema kwamba kama kutatokea msanii ambaye atakwenda msibani hapo kwa ajili ya kuuza sura au kuutafuta umaarufu hatasita kumfukuza.
"Huu msiba ni wetu wote na kama atatokea msanii yeyote na kuja pale kwa ajili ya kutafuta umaarufu nitamfukuza," alisema Steve.
Steve alisema katika msiba huo wasanii wote watahiska katika majukumu mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa Kaburi, Jeneza, Mashada ya Maua, Usafiri pamoja na mambo mengine muhimu katika msiba huo.
Marehemu Adam Kuambiana alifariki dunia Jumamosi asubuhi akiwa katika kuhitimisha filamu yake mpya ya Jojo. Taarifa za awali zilidai kwamba, marehemu Kuambiana siku chache kabla ya kifo chake alikuwa akilalamikia kusumbuliwa na tumbo pamoja na vidonda vya tumbo. Aidha, Stara Thomasi ambaye ni miongoni mwa wasanii waliokuwa karibu na marehemu, alimwambia mwandishi wetu, Edson Mkisi Jr kwamba marehemu pia alikuwa akisumbuliwa na mgonjwa wa Kisukari.


0 Maoni:
Toa Maoni