Kama unafuatilia blog hii jumatatu niliweka habari kuhusu Beyonce na Jay Z walioonekana wanakata mitaa ya New York baada ya tetesi kuzagaa wamemwagaa huku wakiwa na mtoto wao Blue Ivy ambaye nilikudokeza kuwa ameshaanza kutengenezwa muonekano baada ya nywele zake kutengenezwa kwa muundo wa dread...
Basi sasa nywele za Blue zimezua balaa baada yaMwanamke mmoja ambaye tunaweza kumuita mwanaharakati asiye rasmi, Jasmine Tolver wa Brooklyn, New York Marekani akuanzisha harakati/kampeni yenye lengo la kumshinikiza Beyonce kuzichana nywele za mwanae Blue Ivy kwa madai kuwa kuziacha katika hali zinazoonekana ni sehemu ya unyanyasaji au ukosefu wa matunzo bora ya mtoto.
Mwanamke huyo ameanzisha petition kwenye mitandao ambayo inahitajika kukusanya saini nyingi iwezekenavyo ili sauti imfikie Beyonce kwa nguvu.
Mwanamke huyo ameanzisha petition kwenye mitandao ambayo inahitajika kukusanya saini nyingi iwezekenavyo ili sauti imfikie Beyonce kwa nguvu.
Habari kwa hisani ya Times fm Tz


0 Maoni:
Toa Maoni