Ndoa za mastaa Nigeria nazo mgogoro, Tiwa Savage na Ini Edo kwenye list..


Mahusiano na ndoa za mastaa zimeendelea kuyumba na safari hii tunaelekea nchini Nigeri na tunakutana na mastaa Ini Eddo na Tiwa Savage ambao nao inasemekana ndoa zao zimeingia kidudu mtu.

Tukianzia na Tiwa Savage inasemekana hawana mahusiano mazuri na mume wake Tee Billz kisa kikidaiwa ni michepuko huku vyanzo vingine vikiripoti kuwa vipigo ndio sababu. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi inasemekana Tiwa ameajiri meneja mpya anayeitwa Emeka huku akimtosa mumewe ambaye ndio alikuwa meneja.

Tukirudi kwa upande wa Ini Edo ambaye baada ya miaka mitano ya ndoa na mume wake anayeishi US Philip Ehiagwina nao wamebwagana huku bidada huyo akiondoka jina la mwisho la mumewe alilokuwa akitumia kwenye mitandao ya kijamii! tena kwenye Bio aliandika wife/ actress lakini sasa ile wife imetoka!

Tiwa Savage na Emekah
Ini Eddo

0 Maoni:

Toa Maoni