Diamond Platinumz ameonesha jinsi ambavyo penzi lake na Wema Sepetu linazidi kuimarika tofauti na habari zilizokuwa zimesambaa kwenye magazeti hivi karibuni baada ya kumzawadia kichuna wake gari jipya aina ya Nissan Morano kama zawadi ya birthday ambalo lilikabidhiwa kwa Wema na mama mkwe Bi Sandra.
Mwimbaji buyo alishare picha ya gari hilo kwenye Instagram na kumuandikia ujumbe mtamu mrembo wake aliyekuwa miss Tanzania 2006.
Meneja wake pia Martin Kadinda nae alimsapraizi Wema kwa zawadi ya gari la kisasa aina ya BMW na kufanya bidada kuondoka na magari mawili ya zawadi...licheki hapo chini.

0 Maoni:
Toa Maoni