Bwana harusi wa ki-Saudi ameshangaza uma baada ya kumpa talaka mke wake kwenye usiku wa sherehe ya ndoa yao baada ya kuona uso wake kwa mara ya kwanza!
Wawili hao kutoka mji wa Medinah uliopo Saudi magharibi walikubaliana kuoana bila hata kuwahi kukutana uso kwa uso baada kuanzisha uhusiano kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati wa sherehe ya harusi ndipo mpiga picha alipoomba maharusi wapozi kwa ajili ya picha lakini bibi harusi alipofunua shela huku akitabasamu kwa ajili ya kamera bwana harusi alipata mshtuko na kuanza kupiga kelele ''Wewe sio msichana niliyetaka kuoa...sio yule niliyemfikiria mawazori..nisamehe ila sina budi kukupa talaka''
Baada ya kauli hiyo bibi harusi alimwaga machoziakadondoka chini na kuzimia huku waalikwa wakisogea na kujaribu kusuluhisha lakini haikumfanya bwana mkubwa abadili maamuzi yake... mapenzi ya mtandaoni haya!

hahaha, alikuwa anaweka profile pic ya kim kadarshian
ReplyDeleteULIMWENGU WA DIGITAL HUU TAABU SANA.
ReplyDelete