Instagram yaipiga bao twitter kwa watumiaji


Mtandao wa Instagram unaendelea kufanya vizuri zaidi linapokuja swala la mitandao ya kijamii na sasa mtandao huu umefikisha zaidi ya watumiaji milioni 300.

Kwa mujibu wa mmoja wa wamiliki wa Instagram Kevin Systrom aliyetoa takwimu hizi, Instagram imewapiga bao hadi twitter ambayo ina watumiaji 284 kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa wiki 6 zilizopita.

Mtandao huu umeanzishwa miaka minne iliyopita ambapo mbali na kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 300 pia kuna zaidi ya picha na video milioni 70 zinatumwa na watumiaji kila siku.

0 Maoni:

Toa Maoni