Achilia mbali kuwa ni mama lakini pia ana miaka 45 kwa sasa hii haijamfanya mwanamama huyu kuchuja na kupoteza mvuto wake... ndio kwanza anazidi kuwa ng'aring'ari! Namzungumzia Jeniffer Lopezi...J lo.
Mwanamuziki huyu mrembo amepata nafasi ya kupamba jarida la Complex linalokuwa sokoni mwezi february mpaka march akiwa kwenye ubora wa hali ya juu huku akifungukia wanafanya upasuaji kubadili muonekano pia akijibu wale wanaomshambulia kuwa ni mzee na hafai kujianika kujianika kwa sasa.. shuka nayo -->>
"Ina maana siruhusiwi kuwa na mvuto kwa sababu mimi ni mama? Sisemi kuwa ipo siku pia wataniuliza mama kwa nini ulifanya vile! Lakini sidhani pia kama miaka 10 mbele ntaendelea kufanya hivyo pia" Alifunguka Jlo ''Maumbile ya wanawake wegi huko nje ni ya kutengeneza japo si kazi yangu kujaji.''




0 Maoni:
Toa Maoni