HALI MBAYA YA MANDELA YAKATISHA ZIARA YA RAIS ZUMA!


          Watu mbalimbali wanaendelea ku show love kwa Mandela nje ya Hospitali aliyolazwa mjini Pretoria.

Hali mbaya ya Rais mstaafu wa Africa Kusini Nelson Madiba Mandela 94,imesababisha Rais wa nchi hiyo Jackob Zuma kuhairisha ziara yake ya kwenda nchini Msumbiji baada ya kushauriana na madaktari wanaomtibu Mandela.Msemaji wa Rais Zuma,Mac Maharaj amethibitisha kuhairishwa kwa ziara hiyo iliyokuwa ianze leo.

Hali ya Mandela anayesumbuliwa na uginjwa wa mapafu inaelezewa kuwa mbaya zaidi na haijaweza kuimarika tokea amefikishwa Hospitali huko Pretoria.

Watu mbalimbali wamesema kwasasa wako tayari kupokea taarifa yoyote hata kama ni ya huzuni inayomuhusu Mandela japo inaumiza kusikia taarifa za huzuni.

0 Maoni:

Toa Maoni