HISPANIA YAIFUATA BRAZIL FAINALI CONFEDERATIONS CUP!

Timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Confederations Cup baada ya kupata ushindi wa penati 7-6 dhidi ya Italy.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana na dakika 30 za nyongeza nazo hazikumpata mbabe mpaka kwenye mikwaju ya matuta ambako Italy walikosa mkwaju mmoja.

Leonardo Bonucci wa Italy alikosa mkwaju wa penati uliopaa juu ya lango na Jesus Navas wa Hispania akapata mkwaju wake uliowapeleka Hispania fainali na sasa watacheza dhidi ya wenyeji Brazil hapo Jumapili kwenye uwanja wa Maracana.


                                          Raha ya kwenda fainali kwa wachezaji wa Hispania
                                         Jesus Navas akitumbukiza mkwaju ulioipeleka Hispania fainali

0 Maoni:

Toa Maoni