BRAZIL BINGWA CONFEDERATIONS,HISPANIA WAKUBALI KIWANGO!


                                          Neymar akimtesa Casillas kuiandikia Brazil bao la pili
                    Huzuni ya kufungwa kwa wachezaji wa Hispania na kocha wao Vicente Del Bosque...

Timu ya Taifa ya Brazil imefanikiwa kurejesha enzi zake za mataji baada ya kufanikiwa kuitungua Hispania kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Maracana.

Mabao ya Brazil kwenye mchezo huo yalipachikwa wavuni na Fred aliyetupia mawili na moja lililotumbukizwa na Fred huku ikishuhudiwa mkwaju wa penati wa Sergio Ramos wa Hispania ukiokolewa na kipa wa Brazil Julio Cesar.

Michuano hiyo pia imezidi kumng'arisha kinda Neymar aliyefanikiwa kuibuka na tuzo ya mpira wa dhahabu,huku Fernando Torres akiibuka na kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Kwa upande wa kocha wa Hispania Vicente Del Bosque amekubali kuwa Brazil ni timu nzuri na akisema hawana sababu ya kulaumu hali ya hewa ya joto waliyokutana nayo kwenye mji wa Fortaleza.

0 Maoni:

Toa Maoni