Cheki urembo wa kutoboa ulimi na Nelly Kamwelu

Mara nyingi umeshawahi kukutana na kina dada wakiwa wametoboa ulimi na kuvaa kipini pengine ukajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu kuhusu urembo huo..Kutana na nyota wa kibongo Nelly Kamwelu mrembo aliyeshiriki mashindano mbalimbali ya urembo na kufanikiwa kunyakua taji la Miss Universe akiwa na kipaji cha kuimba lakini ni video qeen pia.




Nelly ameongeza madoido ya urembo wake kwa kutoboa ulimi na kupachika kipini.Shughuli hiyo ameifanyia nchini Uingereza mwaka 2011.




Nelly alivutiwa na urembo huo kutoka kwa mwanamuziki Mel B tokea akiwa mdogo.


Anasema kutoboa ulimi kuna maumivu makubwa inahitaji moyo japo unaweza kuwekwa ganzi.Hata yeye aliogopa ila alilazimika kutoboa kwa kuwa alishafika kwa mtoboaji na ulimi ulishawekwa tayari kwa shughuli hiyo..akanikumbusha usemi 'maji ukishayavulia nguo sharti uyaoge!'


Kupitia hapa najua ume enjoy vya kutosha tu!

0 Maoni:

Toa Maoni