Cheki Picha iliyomfanya rapper Kanye West amzimie Kim K

Inaweza ikawa kama utani au ujinga kwa wengine lakini ndio hali halisi..Hii picha hapo chini ya Kim K akiwa na Paris Hilton iliyopigwa mwaka 2006 ndio ilimfanya rapper Kanye West kuzama kimapenzi kwa Kim Kardashian!

Akizungumza na mama wa Kim Kris Jenner kwenye talk show ya mwanamama huyo,Kanye anasema alikuwa anajua Kim anapenda Ku-date na wacheza mpira alitamani kuwa hivyo ili amnase Kim kimapenzi.

Mama yake Kim, Kris Jenner alisema Kanye aliona picha ya familia yao online akaamua kuifanyia photoshoot Picha inamuonesha yupo nyuma ya Kim na kutengeneza kadi aliyo-share na familia hiyo katika sikukuu ya Xmass ili kuonyesha hisia zake.
Picha inayoonesha mchoro wa  mtu nyuma ya Kim aliouchora Kanye..naona alimaanisha kulitakiwa kuwe na uwepo wake hapo haha!



0 Maoni:

Toa Maoni