Wakiwa wamebaki washiriki watano,kwa kanuni za shindano hilo washiriki wawili wakaanza kutolewa na panga hilo likaangukia kwa washiriki kutoka nchini Nigeria Beverly na Melvin kabla ya kutolewa tena kwa Elikem kutoka nchini Ghana na kuwaacha wanadada wawili Cleo na Dillish ambao walijipachika jina la Princes katika siku za nyuma.
Na ilipofika wakati wa kutangazwa aliyechukua kitita hicho cha dola laki 3 Dillish akawa hana upinzani na Cleo akatajwa kutoka na kumuacha mshindi huyo akimwaga chozi la furaha akishinda kuamini kilichotokea.
Wakati washiriki wote wa BBA The Chase walipotangazwa uwepo wao na kupanda kwenye stage wakiwepo washiriki kutoka Tanzania Feza Kessy na Nando,mshiriki kutoka Zambia Sulu akawa wa mwisho kutajwa tena ikionekana kama amesahaulika na alipotajwa uwepo wake akaangusha bonge moja la surprise akaingia na mwanadada Salma na wimbo wake alioufanya kusifia nyumba ya big brother iliyopewa jina la Ruby na kuamsha shangwe.
Huu ndio ushindi wa kishindo wa Dillish
Hivi ndivyo nchi zilivyopiga kura :
Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total: Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.
(Total: 15 Votes)





0 Maoni:
Toa Maoni