Kati ya washiriki watano waliobaki BBA unafikiri ni nani ataibuka mshindi?

Baada ya jana Bimp na Angelo kuaga shinado la BBA The Chase sasa wamesalia washiriki watano mjengoni ambao wameingia fainali.Swali ni je unafikiri kati ya hawa washiriki waliobaki nani ataondoka na kitita cha dola laki tatu sawa na zaidi ya shilingi milioni 450 za ki TZ?

1: Beverly (Nigeria)
Huyu ni mwanadada mwenye bahati sana maana ameweka record ya kutoingia kwenye nomination tangu shindano lilipoanza.Alikuwa na uhusiano na Angelo kijana kutoka Africa Kusini ambaye jana aliaga shindano rasmi.Lakini pia alikuwa na ukaribu sana na Bimp mshiriki kutoka Ethiopia ambaye nae aliaga shindano.Kwa kutogusa machungu ya Nomination hata mara moja unadhani inaweza kumfanya Beverly Kuwa mshindi?

2:Elikem (Ghana) 
Ni m-ghana wa kwanza kuingia fainali tangu mashindano yaanze kwa hiyo kaweka historia katika nchi yake.Ameshanusurika kutoka mara nyingi kwa kuwa ameshakuwa nominated mara tano na kati ya hizo mara mbili alikuwa saved na Head Of House na yeye mwenyewe mara mbili Afrika ilimweka salama.Elikem.Inawezekana nafasi aliyopata ya kuwa Head Of house mara tatu imemuokoa na kumfikisha alipo.Aliwahi kupata strike moja kwa sababu ya ugomvi wake na Nando aliyekuwa mshiriki kutoka Tanzania ambaye alikuwa disqualified baada yaya kutimiza stikes tatu na kuvunja masharti ya BBA.

3:Dillish (Namibia)
Jana alikamilisha idadi ya washiriki watano kuingia fainali baada kuwa saved na kushuhudia Bimp na Angelo wakiaga shindano baada ya kupata kura . Ameshakuwa nominated zaidi ya mara nne na hatimaye anakwenda kuiona fainali.

4:Cleo (Zambia)
 Wengi walijua mshiriki atakayeiwakilisha Zambia mpaka fainali ni Sulu lakini haikuwa hivyo Ice qeen au Cleo kama anavyofahamika ndiye mshiriki kutoka zambia aliyeingia fainali. Ameshasalimika kama mara tatu hivi baada ya kuwa nominated na kudhihirisha uimara wake ni msanii yaani mwanamuziki anafokafoka kutoka Zambia kule.

5:Melvin (Nigeria)
 Ni mshiriki mwingine aliyepata bahati ya kuingia fainali.Alishawahi kujiweka kwenye hatari ya kutoka alipokuwa Head Of House baada kutojiokoa kama wafanyavyo wengine.

0 Maoni:

Toa Maoni