Washiriki hao wawili walikuwa pamoja na mwanadada Dilish kutoka Namibia ambaye yeye amesalimika na kuwa mmoja wa washiriki watano waliokwenda hatua ya fainali.
Kabla ya kutoka washiriki hao wote watatu waliinuliwa na kuambiwa waende kwenye chumba kingine ambako ndiko wangefahamu nani anatoka nani anabaki na wakaingia kwenye chumba hicho maarufu cha Rendezvous.
![]() |
| Bimp |
Mwendeshaji wa kipindi hicho IK akawapa maelekezo ya kwamba atakayetajwa jina lake atatoka moja kwa moja bila kupata nafasi ya kuwaaga wenzake na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Bimp na Angello kuondoka kimya kimya bila mkono wa kwaheri.kutoka kwa wenzao.
![]() |
| Angello |
Washiriki waliobaki kwenye jumba hilo walishangaa kumuona Dilish peke yake huku Bimp na Angello wakiwa wametoka bila ya kuwaaga na mwanadada huyo akachukua fursa ya kuwaeleza wenzake kile kilichotokea huko Rendezvous room.
Washiriki walioingia fainali mbali na Dilish ni pamoja na Melvin na Beverly kutoka Nigeria,Elkem kutoka Ghana na Cleo kutoka Zambia.
Fainali itakuwa Jumapili ijayo August 25 na mshindi atajizolea kitita cha dola laki 3 sawa na zaidi ya shilingi milioni 450 za Tanzania.




0 Maoni:
Toa Maoni