Mchungaji awapiga marufuku wanawake kuweka weaving kanisani

Pastor A.J Aamir ambae ni mchungaji wa kanisa la Resurrecting Faith lililopo Waco Texas,amewaambia waumini wake wasivae au kusukia weaving kwa sababu anaamini wanawake wanaovaa weaving hawaleti picha nzuri na huonyesha kutojikubali

“Wanawake wetu wenye asili nyeusi wanapenda kuvaa weaving na kujaribu kuwa tofauti na uhalisia walionao..Kuwa wewe na jikubali ndio ninachosema” amesema mchungaji Aamir. Naongoza kanisa ambalo waumini wangu wanahangaika kusaka hela kifupi wanahangaika halafu anakuja mwanamke ana weaving kichwani ya dola 300! Hapana siwezi kukaa kimya kuhusu hili" ameongeza mchungaji.

Pastor Aamir anakiri kuwa kalelewa katika familia yenye maadili kwa sababu mama na baba yake walikuwa ni waumini wazuri wa dini.

Pastor Aamir anasema anajua hawezi kuzuia wanawake wote kuvaa/kusukia weaving lakini hawezi kuruhusu hilo.

0 Maoni:

Toa Maoni