Peter Manyika: Kutoka kwenye soka mpaka muziki

Leo Mamu Africa blog inakupa nafasi ya kumjua Peter Manyika ambaye alikuwa kwenye soka na sasa kageukia upande wa pili yaani kwenye muziki.
Peter Manyika alipokuwa katika studio za Times fm
1:Aliwahi kuwa golikipa kwenye timu za Yanga, Mtibwa,Sigara na Timu ya taifa ya Tanzania.Pia amewahi kucheza soka nje.

2:Ana miaka ishirini sasa tangu aanze mambo ya soka.

3:Hajaanza muziki hivi karibu, alianza kitambo na alishatoa album ila akapata safari ya kwenda Shelisheli kwa ajili ya soka hivyo akaacha muziki kwanza na album yake haikutamba maana haikupata promo ya kutosha.
4:Style yake ya muziki inaitwa MAKAMA (Mashariki,Kati,Magharibi). Anasema ameingia rasmi kwenye muziki sasa na album yake ya kwanza inaitwa Wananipeleka puta.Ana wimbo unaitwa Wololo ambao unafanya vizuri na Manabii aliowashirikisha Fid Q na Mad Ice.

Peter Mnyika katika Hatua Tatu ya Times fm
5:Ana mke na watoto wawili na mtoto wake wa kiume Manyika Junior amefata nyayo za baba yake na sasa anachezea kwenye timu ya Taifa ya vijana ya Under 17 kama golikipa chaguo la kwanza.

0 Maoni:

Toa Maoni