Tukio hilo ambalo lilitokea mishale ya saa 2 usiku kwenye gesti ya Green Pau iliyopo maeneo hayo ya Kurasini ilitokana na mchumba wa jamaa (binti) kumtonya jamaa yake kwamba kuna mtu anamtaka kimapenzi.
"Baada ya mchumbaangu kuniambia hayo niliangalia ile namba na kugundua mtu aliyekuwa kimtaka mchumba wangu ni rafiki yangu wa zamani sana tena ni wakufa na kuzikana," alisema jamaa huyo kwa masikitiko.
Alisema kutokana na jamaa huyo kutaka kutembea na mchumba wake na yeye aliamua kumfanyia umafia wa kumuumbua mbele ya jamii ili iwe fundisho kwa wengine.
"Nilikaa nikatafakari sana maana jamaa alikuwa akimtumia mchumbaangu meseji ambazo siwezi kuzisoma hapa maana ni aibu lakini kubwa alikuwa akimtaka mchumba wangu kinyume na maumbile akidai amejaaliwa sana," alieleza jamaa huyo mbele ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Taarifa zinaeleza kwamba baada ya hapo mipango ya kumfumania jaama huyo ilianza kuandaliwa na takribani mara mbili walipopanga kukutana na mchumba huyo wa mtu alichomoa kwa madai kwamba alikuwa akizidiwa na kazi.
Mtangazaji wa Radio Times Fm, Edson Mkisi Jr ambaye alikuwa eneo la tukio saa mbili kabla ya tukio, alishuhudia jamaa huyo akiwa mdogo kama nukta asiamini kilichotokea na kubaki mdomo wazi kama zuzu.
![]() |
| Mfumaniwa mwenye nguo ya ndani akihojiwa na wanahabari akiwemo Edson Mkisi Jr wa times fm mwenye taulo begani. |
"Kiukweli sina la kusema hii ni aibu kubwa sana...mume wangu kila siku anadai hapa pesa za matumizi nauza mkaa ndio tule na watoto kumbe ndio mambo aliyokuwa anayafanya, nashukuru sana," alisema mke huyo mbele ya waandishi wa habari.
![]() |
| Mke wa mfumaniwa akizungumza na waandishi wa habari. |






0 Maoni:
Toa Maoni