Picha: Jionee Uzuri wa Bwagamoyo

Zamani Bagamoyo ilikuwa inaitwa Shamba Mgonela maana yake shamba la minazi na wenyeji waliokuwa maeneo hayo.Baadaye ikabadilika na kuitwa Bwagamoyo kutokana na historia inayoeleza kuwa sehemu ya mapumziko wakati biashara ya watumwa ikifanyika yaani ukifika pale una bwaga moyo wako.Lakini wageni walishindwa kuitamka Bwagamoyo na kuanza kusema Bagamoyo jina lililozoeleka mpaka sasa.

Nilipata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali Bagamoyo mwanzoni mwa mwaka huu na zifuatazo ni baadhi ya picha katika maeneo tofauti niliyopita.
Hili ni kaburi la mtoto wa kike aliyeitwa Sharifa ambaye alipewa karama ya kuombea watu wenye matatizo.Alifariki akiwa na umri wa miaka 12 tu. Kwenye hili kaburi watu wenye matatizo mablimbali hufika kwa ajili ya kuomba na baadhi wenye kuamini hufanikiwa.Ukija kuomba hapa unaahidi sadaka yeyote endapo utafanikiwa .
Hapa panaitwa Caravan Serai ni sehemu ambayo waarabu waliokuwa wanafanya biashara ya utumwa wanafikia kwa ajili ya mapumziko kwa ndani humo.
Hapa panaitwa Ngome Kongwe
Hapa ni sehemu ya msikiti uliotumika kutangaza dini ya kiislamu.Kwenye ngazi pale ni sehemu ambayo Imamu anapanda kwa ajili ya kutoa adhana maana kulikuwa hamna spika na akisimama pale juu sauti yake iliweza kusikika sehemu kubwa Bagamoyo.Pia kwenye ndoo pale ni kisima chenye maji waliyotumia kutawadha wakitaka kuswali.Kisima hiki kwa sasa kina maji ambayo hayajawahi kukauka kwa miaka 500 sasa hata watu wayachote kiasi gani.Maji hayo pia yanaaminika ni tiba kwa watu wenye maradhi mablimbali,kuondoa nuksi n.k kwa hiyo watu hufika kunawa na kuomba matatizo yaondoke,wengine wanayabeba kwenye vyombo na kuondoka nayo kwa ajili ya tiba maana huyaita Maji ya baraka.Kila mtu anaruhusiwa kuchota kwa ajili ya kunywa,kunawa,kuoga na hata kubeba.
 Hayo ni makaburi ya baadhi ya viongozi wa kiarabu wa enzi za utumwa. Wageni mbalimbali hufika hapa kutembea na kujionea.
Mimi pia nilipata nafasi ya kujionea.Makaburi ya viongozi yamewekewa minara na kila kaburi linatofautiana urefu wa mnara kutokana na cheo cha aliyefariki.
Hapa nilikuwa naoneshwa Bandari iliyokuwepo kwa mbele kidogo pamoja na mashamba ya mikoko
Hili ni shamba la mamba ambapo Mamba hufugwa na wageni hupita kujionea
Baadae nilipita baharini kupunga upepo yakhee!

0 Maoni:

Toa Maoni